Habari zenu wadau.
Kijogoo Group for Community Development imeanzisha Blog hii kwa malengo ya kujitangaza na kuzitangaza kazi zetu.
Moja kati ya majukumu yetu ni kuielimisha na kuihamasisha ijiletee maendeleo yao kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli na miradi ya kimaendeleo katika maeneo lakini tunaijengea uwezo jamii hiyo kwa kufanya Ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za Umma ( PETs ) na Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ) ( SAM)
Hivyo tunaombwa kuungwa mkono kwa jitihada na juhudi zetu katika kuisaidia Serikali kwenye maeneo ambayo yenyewe haijafika.
kiufupi shirika hili toka lianzishwe mdau wetu mkubwa aliyetufadhili kwa miradi ni The Foundation For Civil society Ya jijini Dar Es Salaam
Shirika la Kijogoo Group For Community Development limeanzishwa kwa kusudi ya kusaidia jamii kwa kuiweka pamoja kwa minajiri ya kushauriana na kubadirishana mawazo na uzoefu katika kuyatafuta na kuyasimamia maendeleo katika Nyanja na sekta zote kwa lengo la kuinua na kukuza uchumi wa watu kwa kuzingatia makundi yote.
Wednesday, 11 May 2016
MKUKUTA UNAUMUHIMU SANA
MKUKUTA ni neno maarufu katika jamii ya Tanzania toka ulipozinduliwa mwaka 2005. Kirefu chake ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania , MKUKUTA umeboreshwa kutoka katika Mkakati wa kwanza wa kupunguza umaskini wa uliozinduliwa Oktoba mwaka 2000 na unatekelezwa kuanzia 2005 hadi 2010.
Mojawapo ya eneo ambalo MKUKUTA umejikita ni ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini wa kipato. Eneo hili lina malengo sita likiwemo la kupunguza umaskini wa kipato kwa wanawake na wanaume wa maeneo ya vijijini. Inadhamiriwa ifikapo 2010 wanaoishi chini ya mstari wa umaskini wapungue toka asilimia 38.6 hadi asilimia 14.
Kupungua huko kutatokana na wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao ni wakulima wadogo vijijini endapo watajengewa uwezo wa kuongeza tija na kupata faida ndani na nje ya sekta ya kilimo. Kuwezesha kutafuta masoko ya uhakika ya bidhaa za kilimo. Kuwajengea uwezo wa kuongeza thamani mazao wazalishayo ili waweze kupata faida.
Wakazi wa sehemu hizo wajengewe pia uwezo wa kutumia raslimali zinazowazunguka na hivyo Kuongeza michango inayotokana na wanyama pori , misitu na uvuvi katika vipato vya jumuiya za vijijini. Haya yakitekelezwa vyema itakuwa ni rahisi kwa wakazi hao wa vijijini kupunguza umasikini wa kipato na hivyo kukuza uchumi.
Tangu MKUKUTA uanze kutekelezwa kumekuwepo na jitihada mbalimbali za wadau katika utekelezaji wake. Wananchi kila mahali wameanzisha vyama vya kukopa na kuweka (SACCOS). Vyama hivi vinawasaidia wananchi wenye kipato cha chini kupata mikopo inayowasaidia kuendeleza kilimo au biashara zao ndogo ndogo.
Takwimu zilizopatikana zinaonesha hadi mwaka 2007 karibu wajasiriamali wadogo wadogo 20.000 walipatiwa mikopo kutoka kwenye SACCOS mbalimbali nchini ongezeko zaidi linatarajiwa baada ya hatua ya serikali kutoa karibu bilioni moja kwa Mkoa ili kusaidia kuwakopesha wanyonge wasioweza kukopesheka na mabenki.
Kwa muda mrefu kilimo kimekuwa kinakabiliwa na chanagamoto nyingi. Kasi ya kukua kwa kilimo ni asilimi 5 katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Hii inatoa picha inayobashiri kuimarika zaidi sekta hii iwapo mipango iliyopo itatekelezwa na kusimamiwa vizuri. Basi wakazi hao wa vijijini wanaweza kuondokana na umaskini.
Kwa upande mwingine, pato la taifa(GDP) linaendelea kuongezeka. Hii inaashiria uchumi wa nchi kukua. Mfano, mwaka 2006 Pato la taifa lilikuwa kwa asilimia 6.2. Lengo la MKUKUTA linasema ifikapo mwaka 2010 pato hilo liongezeke na kufikia asilimia kati ya sita ana nane.
Kumekuwepo na ongezeko la mapato ya wakazi wa vijijini katika sekta ya ufugaji. Ingawaje bado wafugaji wanafuga kizamani na kuuza mifugo yao bila ya kuongeza thamani, bado ng’ombe waliouzwa nje walifikia thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 2.9 kiasi ambacho ni kikubwa na kinachangia kupunguza umaskini wa kipato vijijini.
Moja ya vikwazo kufikia lengo hili ni miundombinu, katika maeneo ya vijijini hasa barabara na umeme ni kiwazo kikubwa cha juhudi za kujikwamua kiuchumi kwa wakazi wengi wa huko. Barabara zisizounganika zinakwaza usafirishaji wa mazao na kupata tija kwa wakati muafaka. Mazao mengi huozea mashambani hasa wakati wa msimu wa matunda
Umaskini wa kipato vijijini unachangiwa na wakulima kuendesha kilimo cha kujikimu kwa kutegemea mvua, uzalishaji duni, nguvu kazi haba na vitendea kazi duni ingawaje huduma za kilimo cha umwagiliaji zinaonesha kuanza kukua lakini wananchi wengi hawatumii kutokana na ubunifu mdogo na baadhi ya wanaotumia wamefanikiwa.
Mitaji na fursa finyu ya kupata mikopo ni changamoto kwa wakazi wengi wa vijijini. Maeneo ya mijini tatizo linaonekana sio kubwa sana ukilinganisha na maeneo ya vijijini. Ndio maana MKUKUTA umeyatenga malengo ya kupunguza umaskini wa kipato kwa wakazi wa mijini tofauti na wale wa vijijini kwa vile wanahitaji mbinu tofauti.
Matumizi halisi ya nishati ya kupikia ni changamoto kwa wengi. Serikali inasisitiza nishati za umeme na gesi zitumike hasa ili kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kukata miti ya kuni. Kwa wakazi wengi wa vijijini hili bado ni tatizo. Kutokana na gharama za nishati mbadala wengi hawaziwezi huendelea kutumia kuni na mkaa.
Hali ngumu ya maisha hasa umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja unaripotiwa kuongezeka hasa mwaka 2007. Karibu asilimia 82 ya vijana waliosailiwa katika zoezi la kukusanya maoni ya wananchi juu ya MKUKUTA walidai ugumu wa maisha unaongezeka kila siku kutokana na kukosa ajira na kupanda kwa garama za maisha.
Serikali licha ya kuwa na mikakati ya kuboresha miundombinu ya kiuchumi kama vile barabara, huduma za umeme na maji maeneo ya vijijini, ili kuchagiza maendeleo katika maeneo mengi ya nchi hasa vijijini, mikakati hiyo iende sambamba na upatikanaji wa nishati za uhakika na hasa umeme wa jua ambao utachangia kupunguza kazi za sulba.
Viongozi wanapaswa kuhamasisha wakulima vijijini kuzalisha mazao yenye faida kubwa na kuongeza upatikanaji wa nyenzo za kilimo na matumizi sahihi ya teknolojia Suala hili liende sanjari na mbinu za usimamizi wa mavuno katika kaya za vijijini na kukuza miradi inayoongeza thamani katika kilimo,uvuvi mifugo na bidhaa za misituni
Katika lengo hili kuna mikakati kundi zaidi ya kumi na nane iwapo serikali na wadau watahakikisha mikakati kundi hiyo inatekelezwa haraka wananchi wa vijijini wake kwa waume wanaweza kupunguza umaskini wa kipato na kuvigeuza vijiji kuwa kimbilio la watu wengi kuliko ilivyo hivi sasa vijana huvikimbia kuogopa kuzama kwenye umaskini.
Yapo maeneo ambayo wananchi wake hawahitaji fedha kwa ajili ya mitaji ya kuongeza kipato lakini wanakabiliwa na umaskini wa kipato kutokana na sheria ambazo kama zingerekebishwa zingeweza kuwajengea mazingira mazuri ya kuinua hali za maisha yao Ni jukumu la serikali kupitia sheria zenye mapungufu na kuziboresha ili kuleta mafanikio katika kuleta maendeleo kwa taifa.
Mungu ibariki Tanzania
MKUKUTA unalenga kupunguza Umaskini vijijini
MKUKUTA ni neno maarufu katika jamii ya Tanzania
toka ulipozinduliwa mwaka 2005. Kirefu chake ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umaskini Tanzania , MKUKUTA umeboreshwa
kutoka katika Mkakati wa kwanza wa kupunguza umaskini wa uliozinduliwa Oktoba
mwaka 2000 na unatekelezwa kuanzia 2005 hadi 2010.
Mojawapo ya eneo ambalo MKUKUTA umejikita ni ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini wa
kipato. Eneo hili lina malengo sita likiwemo la kupunguza umaskini wa kipato
kwa wanawake na wanaume wa maeneo ya vijijini. Inadhamiriwa ifikapo 2010
wanaoishi chini ya mstari wa umaskini wapungue toka asilimia 38.6 hadi asilimia
14.
Kupungua huko kutatokana na wakazi wa maeneo
hayo ambao wengi wao ni wakulima wadogo vijijini endapo watajengewa uwezo wa
kuongeza tija na kupata faida ndani na nje ya sekta ya kilimo. Kuwezesha
kutafuta masoko ya uhakika ya bidhaa za kilimo. Kuwajengea uwezo wa kuongeza
thamani mazao wazalishayo ili waweze kupata faida.
Wakazi wa sehemu hizo wajengewe pia uwezo wa
kutumia raslimali zinazowazunguka na hivyo Kuongeza michango inayotokana na
wanyama pori , misitu
na uvuvi katika vipato vya jumuiya za vijijini. Haya yakitekelezwa vyema itakuwa
ni rahisi kwa wakazi hao wa vijijini kupunguza umasikini wa kipato na hivyo
kukuza uchumi.
Tangu MKUKUTA uanze kutekelezwa kumekuwepo
na jitihada mbalimbali za wadau katika utekelezaji wake. Wananchi kila mahali
wameanzisha vyama vya kukopa na kuweka (SACCOS). Vyama hivi vinawasaidia wananchi
wenye kipato cha chini kupata mikopo inayowasaidia kuendeleza kilimo au biashara
zao ndogo ndogo.
Takwimu zilizopatikana zinaonesha hadi mwaka
2007 karibu wajasiriamali wadogo wadogo 20.000 walipatiwa mikopo kutoka kwenye SACCOS
mbalimbali nchini ongezeko zaidi linatarajiwa baada ya hatua ya serikali kutoa
karibu bilioni moja kwa Mkoa ili kusaidia kuwakopesha wanyonge wasioweza
kukopesheka na mabenki.
Kwa muda mrefu kilimo kimekuwa kinakabiliwa na chanagamoto nyingi. Kasi ya kukua
kwa kilimo ni asilimi 5 katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Hii inatoa picha inayobashiri kuimarika
zaidi sekta hii iwapo mipango iliyopo itatekelezwa na kusimamiwa vizuri. Basi
wakazi hao wa vijijini wanaweza kuondokana na umaskini.
Kwa upande mwingine, pato la taifa(GDP)
linaendelea kuongezeka. Hii inaashiria uchumi wa nchi kukua. Mfano, mwaka 2006
Pato la taifa lilikuwa kwa asilimia 6.2. Lengo la MKUKUTA linasema ifikapo mwaka
2010 pato hilo
liongezeke na kufikia asilimia kati ya
sita ana nane.
Kumekuwepo
na ongezeko la mapato ya wakazi wa vijijini katika sekta ya ufugaji. Ingawaje
bado wafugaji wanafuga kizamani na kuuza mifugo yao
bila ya kuongeza thamani, bado ng’ombe waliouzwa nje walifikia thamani ya
shilingi za Tanzania
bilioni 2.9 kiasi ambacho ni kikubwa na kinachangia kupunguza umaskini wa
kipato vijijini.
Moja ya vikwazo kufikia lengo hili ni miundombinu, katika maeneo
ya vijijini hasa barabara na umeme ni kiwazo kikubwa cha juhudi za kujikwamua
kiuchumi kwa wakazi wengi wa huko. Barabara zisizounganika zinakwaza usafirishaji
wa mazao na kupata tija kwa wakati muafaka. Mazao mengi huozea mashambani hasa
wakati wa msimu wa matunda
Umaskini wa kipato
vijijini unachangiwa na wakulima kuendesha kilimo cha kujikimu kwa kutegemea
mvua, uzalishaji duni, nguvu kazi haba na vitendea kazi duni ingawaje huduma za
kilimo cha umwagiliaji zinaonesha kuanza kukua lakini wananchi wengi hawatumii
kutokana na ubunifu mdogo na baadhi ya wanaotumia wamefanikiwa.
Mitaji na fursa finyu ya kupata mikopo ni changamoto
kwa wakazi wengi wa vijijini. Maeneo ya mijini tatizo linaonekana sio kubwa sana ukilinganisha na
maeneo ya vijijini. Ndio maana MKUKUTA umeyatenga malengo ya kupunguza umaskini
wa kipato kwa wakazi wa mijini tofauti na wale wa vijijini kwa vile wanahitaji
mbinu tofauti.
Matumizi halisi ya nishati ya kupikia ni
changamoto kwa wengi. Serikali inasisitiza nishati za umeme na gesi zitumike
hasa ili kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kukata miti ya kuni. Kwa wakazi wengi
wa vijijini hili bado ni tatizo. Kutokana na gharama za nishati mbadala wengi
hawaziwezi huendelea kutumia kuni na mkaa.
Hali ngumu ya maisha hasa umaskini wa kipato
kwa mtu mmoja mmoja unaripotiwa kuongezeka hasa mwaka 2007. Karibu asilimia 82
ya vijana waliosailiwa katika zoezi la kukusanya maoni ya wananchi juu ya
MKUKUTA walidai ugumu wa maisha unaongezeka kila siku kutokana na kukosa ajira
na kupanda kwa garama za maisha.
Serikali licha ya
kuwa na mikakati ya kuboresha miundombinu ya kiuchumi kama
vile barabara, huduma za umeme na maji maeneo ya vijijini, ili kuchagiza
maendeleo katika maeneo mengi ya nchi hasa vijijini, mikakati hiyo iende
sambamba na upatikanaji wa nishati za uhakika na hasa umeme wa jua ambao
utachangia kupunguza kazi za sulba.
Viongozi wanapaswa
kuhamasisha wakulima vijijini kuzalisha mazao yenye faida kubwa na kuongeza
upatikanaji wa nyenzo za kilimo na matumizi sahihi ya teknolojia Suala hili
liende sanjari na mbinu za usimamizi wa mavuno katika kaya za vijijini na
kukuza miradi inayoongeza thamani katika kilimo,uvuvi mifugo na bidhaa za
misituni
Katika lengo hili
kuna mikakati kundi zaidi ya kumi na nane iwapo serikali na wadau watahakikisha
mikakati kundi hiyo inatekelezwa haraka wananchi wa vijijini wake kwa waume
wanaweza kupunguza umaskini wa kipato na kuvigeuza vijiji kuwa kimbilio la watu
wengi kuliko ilivyo hivi sasa vijana huvikimbia kuogopa kuzama kwenye umaskini.
Yapo maeneo ambayo
wananchi wake hawahitaji fedha kwa ajili ya mitaji ya kuongeza kipato lakini
wanakabiliwa na umaskini wa kipato kutokana na sheria ambazo kama zingerekebishwa
zingeweza kuwajengea mazingira mazuri ya kuinua hali za maisha yao Ni jukumu la
serikali kupitia sheria zenye mapungufu
na kuziboresha ili kuleta mafanikio katika kuleta maendeleo kwa taifa.
Mungu ibariki Tanzania
Maoni ya Nyerere na uhalisia sekta ya elimu leo
limu Nyerere anasema watu waliopata fursa ya elimu wana wajibu wa kurudi na kulipa fadhila kutokana na kile ambacho wengine wamewafanyia.
Watu waliopata fursa ya elimu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere , mpaka leo wanajivunia elimu hiyo, hali ambayo ni tofauti kabisa na ile wanayopata watoto wetu wa leo.
Ni vigumu kumzungumzia Mwalimu Julius Nyerere leo bila kutaja mchango wake kwenye sekta ya elimu nchini.
Inawezekana kuwa, taaluma yake ya ualimu ndiyo iliyomfanya awe na hamu ya kuhakikisha anaisaidia sekta ya elimu wakati wote wa uhai wake.
Juhudi zake za kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata elimu zilianza hata kabla ya uhuru wa Tanganyika. Kwa mfano, Desemba 20 mwaka 1956 alipopata fursa ya kuzungumza mbele ya Umoja wa Mataifa (UN), kati ya mambo aliyoyazungumzia ilikuwa ni suala la ubaguzi kwenye kupata fursa ya elimu kati ya watoto wa Kitanzania na wale wa Wakoloni.
“Nchini Tanganyika elimu inatolewa kibaguzi. Watoto wote wa Kizungu na wa Kiasia wanakwenda shule ambapo ni asilimia 40 tu ya watoto wa Kiafrika wanaokwenda shule.” Inaeleza sehemu ya hotuba.
Hotuba hii inaweza kutafsiriwa kuwa moja ya viashiria kuwa Mwalimu Nyerere alijali suala la elimu, kwani baadhi ya watu waliopata fursa za kuzungumza mbele ya baraza hilo kumbukumbu hazionyeshi kama walizungumzia suala la elimu.
Japhet Kirilo ndiye alimtangulia Mwalimu Nyerere kwenda kuzungumza UN, Julai 21 mwaka 1952.
Kirilo alitumwa na Chama cha Raia wa Meru (Meru Citizens Union) kwenda UN kudai ardhi ya Wameru iliyokuwa imeporwa na wakoloni, Waingereza.
Maombi ya Kirilo hayakufanikiwa na mpaka leo, eneo kubwa la Meru bado lina mgogoro mkubwa wa ardhi na kubwa zaidi ikiwa imeshikiliwa na watu waliopewa tangu nyakati hizo za wakoloni.
Vivyo hivyo, hata kwenye sekta ya elimu iliyoanza kupigiwa kelele kabla ya taifa hili kupata uhuru, mpaka leo inakabiliwa na changamoto lukuki.
Hata baada ya uhuru, Mwalimu Nyerere aliendelea kupigania elimu, kwenye hotuba zake mbalimbali alizozitoa hakuwa cha kuzungumzia bilasuala la elimu.
Akizungumza juu ya Elimu ya Kujitegemea mwaka 1967, Mwalimu Nyerere alisema: “Kwa kweli nchi huru ya Tanzania ilirithi mtindo wa elimu ambayo kwa njia nyingi ilikuwa haitoshi wala haifai kwa haja za nchi hii. Lakini kulikodhihirika mapema zaidi ni kutokuridhisha kwa elimu.Elimu iliyotolewa ilikuwa finyu. Mwezi Desemba 1961, watu wenye elimu ya kutosha walikuwa wachache mno wala wasingetosha kuendesha Serikali ya siku zile, ukiachilia mbali kazi zingine kama za mipango ya maendeleo zilizokuwa muhimu zaidi.
Idadi ya watoto waliokuwa shule mwaka 1961 haikuwa kubwa ya kutoa matumaini kwamba hali hii ingeweza kurekebishwa haraka.
Zaidi ya hayo, elimu iligawiwa kwa mataifa, ambapo msingi wa madai yetu yote ya uhuru ulikuwa ni kulaani kabisa ubaguzi wa rangi.”
Hadi leo ukijaribu kusoma hotuba zake, utabaini kuwa falsafa yake kwenye suala la elimu, ilijikita zaidi kwenye elimu ya kujitegemea na ile ya watu wazima.
Ama kwa hakika kwa wakati ule, elimu ya kujitegemea iliwasaidia wengi kuwa na mawazo ya kujitegemea wao pamoja na kuliendeleza taifa huku ile ya watu wazima ikiwakomboa mamilioni waliokosa fursa ya elimu wakati wa utawala wa mkoloni.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, mawazo ya Mwalimu kuhusu msingi wa elimu kwa watu wazima, yaliendana sambamba na yale ya wataalamu kama kina Malcom Knowles na J Roby Kidd.
Katika kitabu cha Elimu ya Kujitegemea, Mwalimu Nyerere anasema kati ya makosa matatu yaliyokuwa kwenye elimu ya kikoloni ambayo tuliirithi ni ubaguzi wa rangi katika kutoa elimu.
“Mara tu baada ya uhuru ulianzishwa mpango wa kuunganisha kabisa shule za mataifa yote na ubaguzi kutokana na dini pia ukakomeshwa.
Sasa, mtoto wa Tanzania anaweza kusoma katika shule yoyote ya Serikali, au shule yoyote inayosaidiwa na Serikali katika nchi hii, bila ya kujali rangi au dini yake na bila hofu kwamba gharama ya elimu yake ni kufundishwa dini nyingine,” inaeleza sehemu ya kitabu hicho.
Hata hivyo, wadau wa elimu wanasema kuwa, kwa sasa sifa hii imefutika kutokana na shule za kata ambazo zinawalazimu watoto kusoma shule zilizo kwenye maeneo yao tofauti na zamani ambapo walikuwa wanapangiwa hata nje ya mikoa yao.
Mmoja wa watu waliofanya kazi kwenye sekta ya elimu chini ya Mwalimu Nyerere, Dk Maria Kamm, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru iliyoko Moshi, Kilimanjaro kati ya mwaka 1970 mpaka 1992 anakiri hilo.
Anasema aliweza kuiongoza shule hiyo kwa mafanikio kutokana na sera ya kujitegemea ambayo ilikuwa ikitekelezwa kwa vitendo chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere. “Elimu ya kujitegemea ilijenga jeuri yangu, ilifanya nyote mpate elimu sawa, wote mlikuwa sawa, sote tulifanya kazi bila upendeleo,” anaeleza.
Anaongeza: “Kujitegemea siyo siasa ni kawaida ya Mwafrika, bila kuwa na sera na viongozi kufuatilia utekelezaji wake hatutafika mbali.”
Mwalimu Nyerere pia alichangia ukuaji wa elimu ya juu kwa misingi ya kuwa chachu ya maendeleo na fikra.
Wakati anakifungua Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwaka 1970 alisema, “Chuo kikuu ni taasisi ya elimu ya juu ambayo kwayo watu wanapata mafunzo ya kupanua wigo wa uelewa wao, fikra huru na sahihi, uchambuzi wa matatizo na kuyatatua kwa kiwango cha juu.”
Katika moja ya hotuba alizotoa mwaka 1981, Mwalimu Nyerere alisema watu waliopata fursa ya elimu wana wajibu wa kurudi na kulipa fadhila kutokana na kile ambacho wengine wamewafanyia.
Alisema watu hao ni sawa na wale waliopewa akiba yote ya chakula ili wapate nguvu na kwenda kutafuta kingi zaidi wawaletee wanakijiji wenzao.
Mwalimu Nyerere alisema kuwa, watu hao wasipotimiza wajibu huo, watahesabika kama wasaliti.
Wakati tukifanya kumbukumbu ya miaka 14 tangu kufariki kwake, hatuna budi kukumbuka maneno yaliyomo kwenye hotuba yake ya mwaka 1967 alipokuwa akizungumzia elimu ya kujitegemea.
Alisema: “Elimu inayotolewa Tanzania, kwa watoto wa Tanzania, haina budi itosheleze haja za Tanzania. Haina budi ipande mawazo ya taifa la kijamaa tunalotaka kulijenga.
Haina budi ikazanie kufunzwa kwa wananchi wanaojivunia uhuru na kujitegemea kwa maendeleo yao wenyewe, na ambao wanafahamu faida na shida za kushirikiana.
Elimu haina budi ihakikishe kwamba wale waliosoma wanajitambua kwamba ni sehemu ya taifa na kwamba kwa kuwa wamepata nafasi zaidi, basi wajibu wao kwa taifa ni mkubwa zaidi.
Hili si jambo linalohusu masomo na utaratibu wa shule peke yake. Maadili hufunzwa nyumbani, shuleni na vijijini: Maadili hufunzwa na mazingira ya mtoto anamoishi.
Lakini haina maana shule zetu kukazania kufunza maadili na maarifa yaliyokuwa yanafaa zamani au yanayowafaa raia wa nchi zingine na kumbe elimu yenyewe inapendekeza kuendelezwa kwa hali tuliyoirithi ya kuwa na tofauti baina ya raia na raia wengine.Yafaa watoto wetu waelimishwe kuwa raia wa kesho na watumishi wa wananchi walio sawa, katika taifa tunaloliunda.”
via MWANANCHI
Subscribe to:
Posts (Atom)