MADHUMUNI
- Kuikusanya jamii na kuwaelimisha kwa kuwapatia mafunzo kwa nadharia na vitendo kwa kuwapa ujuzi maarifa yatakayowasaidia ka tika kuendesha maisha yao.
- Waweze kupambana na umasikini kwa njia ya kwa kujituma na kuji saidia wenyewe na kusaidia makundi mengine lengwa wakiwemo watoto,yatima,vijana wazee,wanawake na walemavu
- . Kuanzisha mpango wa elimu kuanzia shule za awali mpaka vyuo ili kuwapa fursa ya kusoma kwa wale wenye mahitaji hayo
- Kuwaweka vijana kuwa pamoja na kupata fursa ya kujadili mambo ya kimaendeleo kwa kubadilishana mawazo kama njia moja wapo ya kujifunza.
- . Kuihamasisha jamii katika kutunza na kuhifadhi mazingira
- Kupiga vita vitendo vyote vinavyoashiria rushwa katika maeneo yote yanayotoa huduma za kijamii pamoja na jamii kuelimishwa juu ya haki zao na kutambua wajibu wao kwa lengo la kuinua utawala bora kupitia utetezi na njia nyingine ikiwa ni pamoja na kutafsiri za sheria kwa kuleta uelewa kwa wote
No comments:
Post a Comment