Katiba Ya Shirika

KATIBA
YA
 KIJOGOO GROUP FOR COMMUNITY DEVELOPMENT
 SEHEMU YA KWANZA

KIPENGELE   1.   JINA LA SHIRIKA

                                 Jina la shirika ni Kijogoo Group For Community Development       
                                 Kijogoo Group For Community Development shirika lisilo
                                  la kiserikali                               

KIPENGELE  2.           SHERIA

2.1    Kijogoo Group For Community Development ni shirika lisilo
la kiserikali au (NGO) lililosajiliwa chini Sheria ya NGO ACT NO- 24/2002

KIPENGELE 3           UTANGULIZI

 Shirika la Kijogoo Group For Community Development limeanzishwa kwa kusudi ya kusaidia jamii kwa kuiweka pamoja kwa minajiri ya kushauriana na kubadirishana mawazo na uzoefu katika kuyatafuta na kuyasimamia maendeleo katika Nyanja na sekta zote kwa lengo la kuinua na kukuza uchumi wa watu kwa kuzingatia makundi yote.

Kijogoo Group for Community Development imeona iko haja ya kufanya ushawishi na uhamasishaji wa jamii ili ijitambue na kuchukua hatua za kupambana na adui Umasikini kwa kufuata sheria na miongozo ya nchi ili kuinua hali za maisha za wananchi na utekelezaji wetu utakua ukiangalia sana vipaumbele vya wananchi wenyewe kulingana na wakati na mahitaji yao.

Katika kutekeleza majukumu yetu tutazingatia makundi yote yakiwemo na vijana, watoto,watu wenye ulemavu,wazee,waishio na vvu/ukimwi,wanawake na hasa waishio katika mazingira magumu hasa umasikini.

Lengo kuu ni kupambana na umasikini kupitia shughuli zinazokubalika na jamii na kufuata sheria inayoelekeza uendeshaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Sisi Kijogoo Group For Community Development kwa niaba ya wapenda maendeleo wote nchini Tanzania kwa nia njema tumeamua kuunda shirika hili na kutumia katiba hii katika kusimamia haki na kutuongoza ili tusiende kinyume na sheria inavyo elekeza.




SEHEMU YA PILI

 KIPENGELE 4.  KUTAJWA KWA KATIBA

    4.1  Katiba inatajwa kwa jina la katiba ya Kijogoo Group For Community   Development na itaanza kutumika baada ya kupokelewa na  kukubalika na   wanachama katika mkutano mkuu wa kwanza wa  wanachama wote waanzilishi na   baada ya kuwa imesajiliwa na mamlaka iliyo na uwezo katika Nchi.

KIPENGELE 5.    AINA

5.1. Shirika hili litajulikana kwa namna mbalimbali kama Kijogoo Group For Community Development.

KIPENGELE 6.    USAJILI

  6.1. Shirika hili litasajiliwa na mamlaka yenye uwezo chini ya sheria ya Mashirika
         yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002

KIPENGELE 7.   MAKAO MAKUU

7.1.Makao makuu ya shirika yatakuwa Morogoro  Tanzania bara
7.2.Shirika litafungua matawi katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kwa kuzingatia 
       mahitaji.
7.3.Anuani ya shirika itakuwa  
      Kijogoo Group For Community Development
      S.L.P. 1198, Morogoro,
      Simu Na. 0754 948767/ 0715 948797
                             
KIPENGELE 8.    LUGHA YA SHIRIKA

  8.1 .Lugha zitakazotumika katika shirika ni
   >    Kiswahili
   >    Kiingereza

KIPENGELE  9. MAMBO MUHIMU

 9.1.     Usawa
 9.2.    Jinsia
 9.3.    Unyenyekevu
 9.4.    Uwazi
          





SEHEMU YA TATU

KIPENGELE 10.          IMANI YETU

 10.1. Kijogoo Group For Community Development tunaamini kwamba Umasikini unasababisha ukiukwaji wa utawala bora usiozingatia uwazi ushirikishwaji na uwajibikaji kutokana na kukosekana kwa usawa na fursa katika uchumi kwa jamii kunapere  kea utamaduni na muundo unaoleta athari kwa makundi hatarishi wa  kiwemo wanawake.watoto,wazee,walemavu na vijana waliopo kati  ka maeneo ya vijijini na mijini

KIPENGELE 11.         DIRA

 11.1. Kuona Jamii yenye uelewa wa kufanya ufuatiliaji wa mapato na  matumizi ya Rasilimali za Umma

KIPENGELE 12       DHIMA

12,1. Kujenga uwezo wa Wananchi na Viongozi kwa Kuelimisha na  kuhamasisha kusimamia na kutekeleza Sheria,Misingi na Kanuni za utawala unaozingatia uwazi ushirikishwaji na uwajibikaji katika   matumizi mazuri ya Rasilimali za Umma kwa njia ya mafunzo   vyombo vya  habari, vipeperushi, majarida na mikutano

KIPENGELE 13.    MADHUMUNI

 13.1. Kuikusanya jamii na kuwaelimisha kwa kuwapatia mafunzo kwa nadharia na vitendo kwa kuwapa ujuzi maarifa yatakayowasaidia ka tika kuendesha maisha yao.

 13.2. Waweze kupambana na umasikini kwa njia ya kwa kujituma na kuji saidia wenyewe na kusaidia makundi mengine lengwa wakiwemo watoto,yatima,vijana wazee,wanawake na walemavu

13.3. Kuanzisha mpango wa elimu kuanzia shule za awali mpaka vyuo ili  kuwapa fursa ya kusoma kwa wale  wenye mahitaji  hayo

13.4. Kuwaweka vijana kuwa pamoja na kupata fursa ya kujadili mambo ya kimaendeleo kwa kubadilishana mawazo kama njia moja  wapo ya kujifunza.

13.5. Kuihamasisha jamii katika kutunza na kuhifadhi mazingira

13.6. Kupiga vita vitendo vyote vinavyoashiria rushwa katika maeneo yote  yanayotoa huduma za kijamii pamoja na jamii kuelimishwa juu ya  haki zao na kutambua wajibu wao kwa lengo la kuinua utawala bora  kupitia utetezi na njia nyingine ikiwa ni pamoja na kutafsiri za sheria kwa kuleta uelewa kwa wote
13.7. Wanawake kupewa fursa na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kimaendeleo na za uzalishaji mali.
KIPENGELE  14.   SHERIA NA UVUJWAJI WA SHERIA

 14.1. Katiba hii sheria na tarabu zilizowekwa chini ya mamlaka yake zita  jumuisha utekelezaji wa kifungu cha sheria za (Sheria ya NGO ACT NO< 24/2002) au sheria nyingine zozote zenye adhira  kama hizo kuhusu mambo ya jamii kwa jumla kwa utekelezaji wa sheria za adhabu za jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zitahusika  popote patakapotakiwa 

SEHEMU YA NNE

KIPENGELE 15     .UANACHAMA

Uanachama katika shirika hili la Kijogoo Group For Community Development uko wazi kwa watu wote wanaotaka kujiunga na shirika bila kujali rangi,kabila,jinsi,elimu ya mtu wala dini.

KIPENGELE 16.      AINA ZA UANACHAMA

16.1Wanachama waanzilishi
16.2Wanachama wanaojiunga baada ya shirika kuanzishwa
16.3Wanachama wa heshima

KIPENGELE 17.     SIFA ZA UANACHAMA

17.1Uwanachama upo wazi kwa yeyote aliyetimiza miaka 18 na kuendelea na awe na
     akili timamu

17.2Aliyetayari kujitolea na kulitumikia shirika kwa muda wake wote anapo hitajika

17.3Anaeguswa na matatizo yaliyomo kwenye jamii

17.4Aliyetayari kujitolea mali kwa kuisaidia jamii iliyoguswa na tatizo

KIPENGELE 18.      MASHARTI NA MAJUKUMU YA WANACHAMA

18.1.Mwanachama atajaza fomu maalumu ya kuomba uanachama

18.2.Akikubaliwa uwanachama atalazimika kulipa kiingilio na ada ya uanachama

18.3.Mwanachama atatakiwa luhudhuria mikutano yote ya shirika inayomuhusu

18.4.Mwanachama lazima aheshimu uongozi uliopo madarakani nakulinda mali za
        shirika

18.5.Mwanachana atatakiwa kutoa ushirikiano kwa uongozi na wanachama wenzie
KIPENGELE 19.   HAKI ZA WANACHAMA

19.1.Mwanachama anayohaki ya kuudhuria vikao

19.2.Mwanachama anahaki ya kuomba na kupatiwa taarif za kiofisi

19.3.Mwanachama ana haki ya kutoa na kupokea maoni kupitia vikaokusaidia na kusaidiwa anapopatwa na matatizo kwa kupata huduma zitolewazo na shirika kwa makundi lengwaMwanachama anayohaki kuajiliwa katika shirika kwa nafasi yoyote ambayo atakuwa na ujuzi nayo.

KIPENGELE 20.    UKOMO WA UANACHAMA

20.1. Kujiudhuru mwenyewe kwa hiyari yake

20.2. Kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu kwa kuvunja sheria,masharti au makosa
         makubwa yasiyokubalika na jamii

20.3. Kufariki dunia

KIPENGELE 21      MATAWI YA SHIRIKA

21.1 Shirka linaweza kufungua matawi popote katika mikoa ya Tanzania Bara kama
         itaonekana kuna haja ya kufanya hivyo kulingana na ma mahitaji ya shirika.

21.2.Kila tawi litafanya kazi kwa kutumia katiba hii kwa utaratibu uliopoila watazingatia
        mahitaji yao kwa wakati uliopo

21.3.Tawi lolote litakalo omba ruzuku au kupatiwa ruzuku lazima makao makuu ifahamishwe kuhusiana na hilo na katika maombi ya kuomba ruzuku mahala popote lazima barua ya utambulisho wa kutambuliwa kwa maombi hayo itolewe na makao makuu kuthibitisha kuwa maombi hayo yanafahamika na makao makuu.

21.4.Uongozi wa matawi utachaguliwa kwa kufuata taratibu za katiba hii na viongozi kutoka makao makuu watakuwa wasimamizi wakuu katika chaguzi hizo.

21.5.Matawi yote lazima yawe akaunti ya benki kwa benki watakayokubaliana kwenye vikao vyao,na lazima jinsia izingatiwe katika kuteua watia saini benki.

21.6.Matawi yote watawasilisha taarifa zao za kila robo mwaka makao makuu kwa ajili ya kuunganisha taarifa na kuwa kumbukumbu zitakazo saidia utendaji kazi wa kila siku.






SEHEMU YA TANO

KIPENGELE 22       MUUNDO WA SHIRIKA

22.1. Kutakuwa na Mkutano mkuu

22.2. Kutakuwa na Bodi ya Shirika

22.3. Kutakuwa na Sekretarieti

22.4. Mwenyekiti

22.5. Mkurugenzi

22.6. Mtunza hazina

22.7. Afisa Miradi

22.8. Afisa ufuatiliaji na Tathmnini

KIPENGELE 23.   VIONGOZI WA SHIRIKA

23.1.Viongozi wote wa shirika  kuanzia mwenyekiti,Mkurugenzi,mwekahazina na afisa miradi watachaguliwa na mkutano mkuu isipokuwa nafasi ya Afisa Ufuatiliaji na Tathmini itateuliwa kulingana na sifa na utaalamu.

23.2.Viongozi wote watakaa madarakani kwa muda wa miaka 5 na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka 5 (miongo 2) baada ya hapo anaweza kuchaguliwa kwa kubadilisha nafasi ya uongozi

KIPENGELE 24.    MWENYEKITI

24.1. Atachaguliwa na mkutano mkuu na ataongoza vikao vyote

24.2. Atasaini mikataba yote shirika ya ndani na nje

24.3. Ndiye msimamizi mkuu wa shirika

24.4. Ataongoza mikutano yote ya shirika
               
24.5. Atakuwa na mamlaka ya kuidhinisha wa malipo na mdhibiti mkuu wa mapato ya
         shirika
24.6. Atawajibika kwenye  Bodi na Mkutano Mkuu



KIPENGELE 25. MKURUGENZI

25.1.Atakuwa afisa mtendaji mkuu wa shirika na ndiye katibu katika vikao vyote
25.2.Atakuwa msemaji na mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za shirika
25,3.Msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za kila idara shirika
25.4. Atatafuta vyanzo vya mapato miradi ya kuelimisha na ya uzalishaji mali.kwa jamii
25.5 Atapitia na kuandaa mikataba itakayoingiwa na shirika kati ya shirika na wafadhili
        au shirika na watoa huduma ndani ya shirika na wanaotoka  nje
25.6 Atasaini mikataba yote ya shirika baada ya kujiridhisha
25.7 Ataidhinisha malipo yote yatakayoitahijika kulipwa baada ya kujiridhisha
                      
KIPENGELE 26.    MWEKA HAZINA

26.1. Atachaguliwa na mkutano mkuu
26.2. Atashughulikia maswala yote ya fedha na kutunza vitabu vya fedha na daftari la
         mali za kudumu za shirika
26.3. Awe mbunifu na uwezo wa maswala ya kifedha
26.4. Ataandaa Hati za malipo na kufanya malipo baada ya hati ya malipo kuidhinishwa
         na mkurugenzi ama atakae kaimu
26.5. Atafuata mwongozo wa fedha unavyoelekeza katika kutimiza majukumu yake
26.6  Atawajibika kwa Mkurugenzi

KIPENGELE 27     AFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI

27.1.Atachaguliwa ama kuteuliwa na mkutano mkuu baada ya bodi kuridhia
        mapendekezo ya sekretarieti.
27.2.Atashughulikia maswala yote ya utafiti,ufuatiliaji na Tathmini
27.3.Ataandaa fomu /dodoso za zitakazotumika kwenye ufuatiliaji na Tathmini
27.4.Atatunza taarifa zote zitokanazo na Ufuatiliaji na Tathmini
27.5.Atamshauri Mkurugenzi njia na mbinu ya kupata matokeo na Atawajibika kwa
         Mkurugenzi

KIPENGELE 28.   AFISA MIRADI

28.1.Atachaguliwa ama kuteuliwa na Mkutano mkuu baada ya  Bodi kuridhia
         mapendekezo ya sekretarieti.
28.2.Atakuwa na kazi ya kuandaa maandiko ya miradi na kuiwasilisha kwa Wafadhili na
        wahisani  kutafuta ruzuku na misaada  ya kuwezesha kutekeleza Miradi ya kijamii
28.3.Atatafuta wafadhili wa ndani na nje
28.4.Ataandaa,kutekeleza,kusimamia  miradi yote itakayoteke lezwa na shirka
28.5.Atandaa taarifa zote za utekelezaji wa mradi,matokeo ya mradi ulio tekelezwa kwa
        kupitia taarifa ya ufuatiliaji baada ya utekelezaji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi
28.6.Atawajibika kwa Mkurugenzi



SEHEMU YA SITA

KIPENGELE  29.      VIKAO

29.1MKUTANO MKUU

29.1.Kutakuwa na mkutano mkuu wa shirika wa wanachama wote wakiwemo waanzilishi Viongozi na Wawakilishi toka katika matawi yetu yote yaliyofunguliwa maeneo mbalimbali.

KIPENGELE 30.        KAZI YA MKUTANO MKUU

30.1.Kuchagua viongozi wa shirika na kupitisha majina ya wajumbe wa Bodi na kuridhia mapendekezo ya Bodi kuhusu nafasi za watendaji waliotajwa kwenye katiba hii ambo watakuwa ni wajumbe wa sekretarieti (Wakuu wa Idara )

30.2. Itapitisha mpango Mkakati wa miaka mitatu, Mpango kazi wa mwaka na Bajeti shirika kwa mwaka unaofuata au   inategemea maamuzi ya wanachama kulingana mazingira ya kazi yanavyoonekana

30.3. Itajadili na kupitisha/kuthibitisha majina ya wanachama wapya
30.4. Kupokea taarifa ya kazi ya mwaka zilizofanywa na shirika ikiwemo taarifa za fedha
         na za utekelezaji
30.5.Kusimamia maadili na kupokea mapendekezo ya Bodi juu ya adhabu kwa wanachama wenao kutwa na makosa


KIPENGELE 31.   SEKRETARIETI

31.1.Kutakuwa na Sekretarieti ya shirika ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia kazi za kila siku za shirika,idadi ya wajumbe ni 5 ambao wane ni viongozi waliochaguliwa na mmoja kutoka miongoni mwa wanachama

KIPENGELE 32.     KAZI ZA SEKRETARIETI

32.1.Kusimamia na kutekeleza kazi za kila siku za shirka wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji
32.2.Kuandaa na kupitia ripoti za kila idara kwa kazi zinazofanywa kila siku na kuboresha pale panapoonekana kuna haja ya kufanya hivyo.

32.3.Kuandaa rasimu ya mpango wa kazi wa shirika na rasimu ya bajeti ya kila mwaka na kuiwasilisha kwenye bodi kwa mapitio,maboresho au marekebisho na kupelekwa kwenye mkutano mkuu kwa kuidhinishwa.
32.4.Kufanya marejea kulingana na mwongozo wa fedha na bajeti elekezi iliyopitishwa kila baada ya miezi mitatu na kuwasilisha mapendekezo kwenye Bodi
KIPENGELE 33.     BODI YA WADHAMIN

33.1.Kutakuwa na Bodi ya wadhamini ya shirika itakayoteuliwa na Sekretarieti na kupitishwa na mkutano mkuu na wajumbe  wake watakuwa watu wenye uwezo wa kifikra, kuheshimika na wenye maadili mema  kwa jamii

KIPENGELE 34.    KAZI ZA BODI YA SHIRIKA

34.1. Kuwa chanzo cha mapato kwa kutafuta wafadhili na wahisani wa ndani na nje wa kuwezesha utekelezaji wa miradi

34.2.Kuangalia mwenendo wa uendeshaji wa shirika kuanzia kazi na majukumu wa watumishi hadi maadili kwa  wanachama.
34.3.Kupitia rasimu zote ikiwemo za Mpango Mkakati,Mpango kazi na rasimu ya bajeti  inayoandaliwa na sekretarieti kwa maboresho na kuiwasilisha kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kuidhinishwa.

34.4.Kuushauri uongozi chini ya Mkurugenzi na idara zake namna bora ya uendehaji wa shirika ili kuleta tija na ufanisi wa kazi.

34.5.Itakuna mara 2 kwa mwaka kwa ajili kufanya vikao vyao ila inaweza kukutana kwa vikao dharula muda na wakati wowote na itachagua mwenyekiti kutoka miongoni mwao na Mkurugenzi na Mwenyekiti wa shirika wanaingia moja kwa moja.

KIPENGELE 35.    MKUTANO MKUU WA MWAKA

35.1.Mkutano mkuu wa mwaka wa shirika ndicho chombo kikubwa cha maamuzi chenye mamlaka ya kupitisha na kuidhisha kutumika kwa  sera,Mipango na Bajeti kama katiba hii ilivyotafsiriwa

35.2.Utakuwa na mamlaka ya kuamua maswala yote yatakayoletwa na Bodi,Sekretarieti na Wanachama au mwachama yoyote washirika au mjumbe wa bodi kulingana na taratibu zilizoelezwa kwenye katiba hii

35.3.Mkutano mkuu wa mwaka utakuwa ukifanyika kati desmba na januari  ya mwaka unaofuata

35.4.Agenda za mkutano mkuu zitatokana na kikao cha Sekretarieti na kugawiwa kwa wanachama wote mwezi mmoja kabla ya mkutano kupitia na kuingiza maoni mapya yatayozungumzwa kwenye mku tano 

35.5.Itatoa taarifa ndani ya siku 21 kwa kubandikwa kwenye mbao za mata ngazo na kuzisambaza kwa wanachama wote kwa maandishi kueleza tarehe na mahali patakapofanyika mkutano na agenda za mkutano mkuu na shughuli za mkutano mkuuzitakuwa ni zile zilizotajwa kwenye agenda

KIPENGELE 36.   VIKAO VYA SEKRETARIETI

36.1. Vikao vya Sekretarieti vitakutana mara moja kila baada ya  miezi mitatu

36.2. Itatekeleza majukumu yake kama ilivyoelekezwa kwenywe katiba hii

36.3. Itashughulikia mambo yote ambayo yanahitajika kuangaliwa baada ya Bodi na
         mkutano mkuu kutoa maagizo kwenye Vikao vyake.

36.4. Itakuwa  na taarifa ya siku 14 kwa wajumbe wa mkutano mkuu

36.5. Itafanya vikao vya dharula pale itakapoamuliwa kufanya hivyo

KIPENGELE 37.    MKUTANO  MKUU WA DHARURA

37.1.Kutakuwa na mkutano mkuu maalumu utakaohitishwa kwa kutoa Taarifa ya dharura kwa wanachama wote kwa kuhudhuria kutokana Na udharura wake kama inavyoelezwa na katiba hii.

37.2.Itafanya marejeo kupitia Mipango iliyopo,Sera,Kanuni na Bajeti baada ya kupokea taarifa ya utendakazi mbovu wa wakuu wa idara katika kutimiza majukumu yake ili kurekebisha kasoro zinazojitokeza kabla mambo hayaja haribika zaidi na kuchukua hatua zinazo stahiki ili kurudisha ubora na ufanisi wa kazi.

37.3.Kuchukua hatua za haraka pindi itakapo pokea taarifa zisizo za kawaida za mwanachama kutoka bodi na kuchukua hatua kabla ya kusubiri mkutano mkuu wa mwaka.

37.4.Kujadili kwa kina taarifa za mfadhili anyetaka kulifadhili shirika kwa kutoa ruzuku ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa za upokeaji wa ruzuku na namna ambavyo Uongozi ulivyoingia mkataba/mikataba,ili nalo litafanyika mapema tu baada ya kufanikiwa kupata ruzuku na haitosubiri hadi mkutano mkuu wa mwaka uitishwe.














SEHEMU YA SABA

KIPENGELE 38.      USIMAMIZI WA FEDHA NA MWAKA WA FEDHA

38.1.Mwaka wa fedha wa shirika la Kijogoo Group For Community Development  utaanzia januari na kuishia tarehe 31 desemba kila mwaka (miezi kumi na mbili)

KIPENGELE 39.     VYANZO VYA FEDHA

39.1.Mapato ya shirika yatatokana na ada za mwaka za wanachama,viingilio vya wanachama.

39.2.Ruzuku kutoka Taasisi za ndani na nje,kupewa na wahisani,misaada,kuchangishana wanachama,zawadi,kutoka kwa watu binafsi,taasisi za ndani na nje ya nchi.

KIPENGELE 40.    MATUMIZI YA FEDHA

40.1.Kulipia kodi za ofisi,kulipia maji na umeme na  kununulia vifaa na samani za ofisi pamoja na kununulia shajala za ofisi.

40.2.Kugharamia  mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wananchi katika mipango,kusimamia na kufuatilia matumizi ya rasilimali katika  kuitekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao

40.3.Kufuatilia shughuli zilizotekelezwa na kufanya vikao vya Tathmini kupima matokeo kwa shughuli za  miradi iliyotekelezwa kwa jamii  Ili kuona  hali ya tatizo ya tatizo lililoshughulikiwa ndani na baada ya utekelezaji wa mradi/miradi.

KIPENGELE 41.   FEDHA

41.1 Mapato yote ya shirika yatapelekwa benki kwa hifadhi kwenye akaunti ya shirika ambayo itaendeshwa kwa saini tatu na mbili kati ya hizo  zitatoa fedha benki kwa akaunti ya saving na kusaini hundi.

41.2 Mwekahazina atatoa taarifa ya fedha zilizopo kwa Sekretarieti na Sekretarieti itaanda taarifa hiyo na kuiwasilisha kwenye Bodi kwa mapitio na kisha kurudishwa kwa Mkurugenzi kwa matumizi. na malipo yote yatalipwa kwa kutumia fomu ya Hati ya malipo iliyoandaliwa na mwekahazina na kupitishwa na mkuu wa idara na kuidhinishwa na Mkurugenzi au   Mwenyekiti au yoyote aliyekaimu nafasi ya Mkurugenzi.

41.3 Kutakuwa na ukaguzi wa fedha za shirika kwa kila mwaka kwa kuanda liwa na Sekretarieti na taarifa hiyo ya ukaguzi itawasilishwa kwenye Bodi na bodi itaipitia kuona kama iko sawa tayari kwa ukaguzi na itapendekeza mkaguzi wa kukagua mahesabu na kuiwasilisha kwenye mkutano mkuu kwa kupata idhini na Baraka na kupitia hilo mweka hazina atalazimika kutunza vitabu vyote vya fedha zikionyesha zilivyopokelewa na  kutumika pamoja na vocha zote za malipo pamoja na vitabu vya risiti

KIPENGELE 42.    RIPOTI YA UKAGUZI

42.1 Mkutano mkuu utaamua kuhusu mkaguzi wa hesabu za shirika baadaya Sekretarieti kuwasilisha majina ya wakaguzi wenye sifa kwa Bodi na bodi kupeleka mapendekezo hayo kwenye mkutano mkuu.

42.2 Maelezo ya mapato

42.3 Mizania

42.4 Mabadiliko katika usemi

42.5 Maelezo ya hali ya kifedha

42.6 Maelezo ya mtililiko wa fedha tasilimu

42.7 Pamoja na ripoti ya ukaguzi na uchunguzi wa utendaji ,bodi ya Wadhamini ya Kijogoo Group For Community Development  itakuwa na utaratibu wa kufanya ukaguzi wa  Muda maalumu kwa uongozi kwa kufanya marejeo ya miongozo,sera na Bajeti kuhusu taratibu za utendaji kwa kuzuia kuendelea kwa mapungufu yoyote yanayoweza kutokea kwa kuonekana mapema katika kipindi cha mwaka

42.8. Baada ya kukamilika kwa ukaguzi na taarifa ikiletwa ofisi sekretarieti itaipitia na kuiwasilisha kwenye bodi na bodi baada ya kupokea itaipitia na kuiwasilisha kwenye mkutano mkuu wa wanachama ili waipitie na kama kulikuwa na mapendekezo yoyote kuhusu ripoti hiyo mkutano mkuu utaamua ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotokana na dosari au changamoto inayopelekea kushuka kwa ufanisi katika matumizi ya fedha au kama haijalidhishwa na mkaguzi aliyendekezwa kufanya kazi hiyo kwa kuwa haina ubora unaotakikana.

42.9. Na ikitokea mkutano mkuu haijaridhiwa na taarifa iliyotolewa na mkaguzi wa hesabu inaweza kuzipeleka hesabu hizo kwa mkaguzi mwingine kama kutakuwepo na fedha ya kufanyia shughuli hiyo













SEHEMU YA NANE

KIPENGELE 43. MAREKEBISHO YA KATIBA,KUVUNJIKA KWA SHIRIKA

·           MAREKEBISHO YA KATIBA

43.1. Katiba itarekebishwa na mkutano mkuu ikifuatiwa na taarifa ya siku ishirini na moja (21) kwa kusudi la kufanya marekebisho ya katiba itakayotolewa kwa wanachama Taarifa lazima ijumuishe marekebisho maalumu ambayo yatasomwa na kujadiliwa sana na wanachama kabla ya kufanyika mkutano wa marekebisho.

43.2. Koramu ya wajumbe wa mkutano mkuu watakao pitisha mabadiliko ya katiba lazima iwe mbili ya tatu( 2/3  ) ya wanachama wote.
.
43.3. Maamuzi ya kurekebisha katiba yatakuwa halali kwa kwa kuungwa mkono na robo tatu ya (  3/4  ) ya wanachama wote.

·         KUVUNJIKA SHIRIKA

 43.4.  Shirika hili linaweza kuvunjika kwa hiyari na kwa maamuzi yatakayo pitishwa kwa pamojana theluthi mbili ya wajumbe wote katika mkutano mkuu utakaoitishwa kwa kusudi hili.

43.5 Taarifa juu ya mkutano huu itatolewa kwa wanachama wote ndani ya siku ishirini na moja(21)kabla ya tarehe ya mkutano mkuu.

43.6 Uamuzi wa kuvunja shirika utakuwa umepitiwa na bodi ya wadhamini ya shirika  na kuteua mufilisi na itatoa ya kuhusu mali za shirika na namna ya kulipa madeni ya ndani na nje ya shirika kama yapo.

43.7.Baada ya kulipa madeni yote kama yapo mali zilizobaki zitagawanywa kwa mashirika ya kijamii yenye malengo yanayofanana na sheria,taratibu zilizowekwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo yakiserikali (NGO) ya mwaka 2002

·           MUHURI WA SHIRIKA

43.8. Muhuri wa shirika hili utakuwa ni Kijogoo Group For Community Development.

43.9 Muhuri ni nyaraka nyeti utahifadhiwa chini ya ulinzi wa Mkurugenzi kwa muda
        wote.

43.10 Muundo wa muuri wa shirika utakuwa wa duara au yai kimaumbile  kutokana na
          mapenzi ya wanachama



SEHEMU YA TISA


44.0  UMUHIMU WA URASIMISHAJI JINSIA KATIKA PROGRAM
                     ZA ASASI.
                                
44.1.Kuongeza ushiriki na ushirikishwaji wa wanawake na makundi mengine ya pembezoni katika utekelezaji wa program za ndani ya asasi na nje ya Asasi.

44.2.Kuimarisha usawa na uwiano wa mgawanyo wa majukumu ndani na nje ya Asasi.

44.3.Kuongeza fursa za uongozi kwa wanawake wanachama wa Asasi.

44.4.Kuimarisha utetezi wa haki za mwanamke na makundi ya pembezoni.

44.5.Kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa program za Asasi.

44.6.Kuwa na utaratibu maalum wa ndani ya asasi wa namna ya kupambana na na changamoto za ukiukwaji wa haki za kijinsia katika utekelezaji wa program za Asasi na namna ya kuzitatua.

45.0 UMUHIMU WA KUWA NA SERA/MWONGOZO WA FEDHA  KATIKA
         PROGRAM ZA ASASI.

45.1. Sera za usimamizi wa fedha(Financial Management Policy) katika Asasi hii kimsingi ni mwongozo unaojumuisha sera za kihasibu ,mifumo pamoja na taratibu zote zinazozingatiwa katika kutunza na kusimamia fedha za Asasi.Mwongozo huo unatengenezwa kwa ajili ya kusimamia fedha za asasi na kuwaelekeza wafanyakazi taratibu zinazopaswa kufuatwa wakati wa kufanya miamala ya fedha katika Asasi.Lakini pia kuwezesha asasi kukidhi matakwa ya sheria na taratibu za nchi pamoja na kudhiirisha kuwa Asasi ina mfumo bora na thabiti ya kiuongozi.

46.0. UMUHIMU WA KUWA NA SERA YA AJIRA  KATIKA PROGRAM ZA
         ASASI.

46.1. Lengo la kuwa na Sera hii ya ajira ni kuongoza katika maswala mazima ya yanayohusu ajira kwa kuwa na mfumo wa kisheria utakaosaidia kuleta mahusiano ya ajira yaliyo bora,ya usawa na yenye viwango sahihi vya misingi ya kazi na pia kuweka mfumo wa kutatua migogoro ya ajira kwa njia ya usuluhishi na upatanishi na kumfanya kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake.


KIPENGELE 47.           MCHANGANYIKO WA MADARAKA

47.1..Kuwekana sawa endapo itatokea hali ya kutoelewana(malumbano)

47.2.Mlalmikaji hatokuwa mjumbe

47.3.Bodi itahusika katika kulisimamia hilo

47.4.Mlalamikaji lazima aikubali kamati ya usuluhishi

47.5.Waamuzi wa migogoro watazingatia vipengele vya sheria za jamuhuri ya muungano
         wa Tanzania.

47.6.Tafsiri ni chombo cha juu kwa kusudi la kutafsiri vipengele vya  sheria hii kitakuwa
        ni bodi ya wadhamini.
.

*********************MWISHO****************************


 SEHEMU YA KUMI

KIPENGELE  48.           KUKILI

48.1.Sisi ni mkusanyiko wa watu mbalimbali ambao majina yetu na saini zetu zimeonyeshwa ikiwa ni wanachama waanzilishi tunatambua kuwepo katika shirika hili kwa kufuata katiba kama ilivyotolewa.

 NA.
JINA LA MWANACHAMA/ANUANI/SIMU
SAINI
1
AMIRI DOTTO

2
RUKIA SELEMANI

3
RAMADHAN  SAIDI

4
SADA JUMA

5
TADEI HAFIGWA

6
ADHA KASIMU

7
AGNES  HAULE

8
MWAJUMA JULIUS

9
SAIDI DUDU

10
SALUMU OMARY

11
MWAGAIANI AMIRY

12
ALLY KIZIGO

13
MARIAM  MAMBO




1 comment: